Mwili wawasili kisumu

Na Laillah
Mohammed

Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Amollo Odinga umewasili mjini Kisumu
katika eneo la magharibi mwa Kenya na tayari umefikishwa katika uwanja wa
michezo wa Jommo Kenyatta Mamboleo.

Raila
alianza safari yake ya mwisho duniani kutoka uwanja wa kimataifa wa Jommo
Kenyatta jijini Nairobi ambapo alibebwa na ndege ya kijeshi aina ya SPARTAN
kutoka kambi ya jeshi la nchi kavu lnalopakana na uwanja wa JKIA.

Shughuli
nzima inaongozwa na jeshi la Kenya KDF ambapo maafisa wa kuu wa jeshi
wamesimamia usafiri wa mwili huo ambao uliwasili katika uwanja wa kimataifa wa
ndege wa Kisumu mwendo was aa moja unusu asubuhi.

Ulipokelewa
na Meja Jeneali Jospeh Nyaga ambaye ni Afisa msimamizi wa kambi zote za jeshi
la nchi kavu katika ukanda wa magharibi mwa Kenya. Luteni Kanali Baraza ambaye
ni msimamizi wa maafisa wa jeshi wanaoulinda na kuubeba mwili wa Odinga,
alishuka kwenye ndege kwanza na kukikongoza kikosi chacke cha mafias wenye
hadhi ya Meja kuandaa jeneza hilo kwa usaidizi wa maafisa wengine wa kijeshi.

Shughuli ya
kuondoa mwili kutoka kwa ndege hilyo ya usafiri wa mizigo na wanajeshi kwa
shughuli zao za kawaida hapa nchini na vitani, ilikuwa na utaratibu uliofuatwa
kwa ufasaha huku wanajeshi wakihakikisha kwamba yote yanakwenda vyema.

Baada ya
karibu nusu saaa jeneza lilisukumwa kwa kigari chenye magurudumu mawili makubwa
cha kubebea maiti na kupitishwa kwenye angatua hadi upande wa pili ambapo ndege
nyingine ya kijeshi aina ya helikopta ya Bell UH -1 ilikuwa inasubiri kuupokea
mwili na kuubebba hadi uwanja wa michezo wa Jommo Kenyatta Mamboleo ambao
ulikuwa umejaa waombolezaji walioanza kufika pale kuanzia saa kumi za alfajiri.

Ndege hiyo
ambayo ilipaa angani kwa muda mfupi tu, kama dakika 8 hivi, wengi wakishangaa
kwa nini hatua hiyo ikachukuliwa na serikali.

Huenda idadi kubw aya watu
iliyopo kwenye barabara kuu ya kutoka uwanja wa ndege wa Kisumu ni mkubwa na
vitengo vya usalama havingetaka hali kama iliyoshuhudiwa siku ya Alhamisi
kutoka uwanja wa ndege wa Jommo Kenyatta hapa Nairobi kurejelewa.

Wananchi
walisimama kando kando ya barabara nje ya uwanja wa Kisumu wakiwa na matumaini
ya kuuona mwili ukipita barabarani ila wengi watapata fursa ya kumuaga Raila
mwanzo tu shughuli hiyo itakapoanza rasmi hapo mamboleo.

Wakenya watautazama
mwili kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na mbili jioni, ambapo Raila Odinga
ataanza safari ngumu kabisa ya kuelekea alikozaliwa kule Bondo usiku wa leo na
kulazwa katika boma lake la OPODA FARM alikoishi na familia yake.

Odinga
atazikwa kando ya baba yake Jaramogi Oginga Odinga – aliyekuwa Makamu wa Rais
wa kwanza wa Kenya na aliyefariki 1994. Familia imesema kwamba baada ya ibada
ya mazishi itakayoandaliwa Jumapili, ni watu wachache tu watakaoingia katika
eneo la makaburini na kushuhudia mwili wake ukishuhswa chini na kuzikwa.

Wananchi
watashuhudia shughuli hiyo kwenye runinga kubwa kubwa ambazo zitawekwa katika
shule za msingi na upili ambazo ziko karibu na makazi ya KANGO’ KA JARAMOGI
ambayo ni boma la mzee Jaramogi na makao ya familia kubwa ya Odinga.

Raila
ambaye alikuwa mwanasiasa nchini Kenya aliye na tajriba wa zaidi ya miaka 35,
alihudumu kama Waziri Mkuu kati ya 2008 na 2013 ambapo aliwania Urais na
kuminyana na Uhuru Kenyatta aliyeshinda uchaguzi huo.

Atakumbukwa
kwa mchango wake wa mabadiliko ya kikatiba, uanaharakatiw ake wa kutetea haki
za waKenya na juhudi zake za upatanishi ndani nan je ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *