Chama Cha Makini kimetoa rai kwa Watanzania kutoshabikia au kushiriki maandamano yanayohamasishwa kufanyika siku ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, na badala yake wajitokeze kwa wingi kupiga kura kisha kurejea majumbani kusubiri matokeo kwa amani.

Kauli hiyo imetolewa na mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho, Coster Jimmy Kibonde, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kaburi la hayati John Pombe Magufuli, akiwa ameambatana na mgombea urais wa Zanzibar na mgombea mwenza wa chama hicho.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *