#HABARI: Chama cha Mapinduzi kupitia mgombea mwenza nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Emmnauel Nchimbi, akiwa katika maeneo ya Kilosa, Mikumi na Kilombero mkoani morogoro kunadi sera na kuomba kura kwa wananchi amesema, chama hicho katika kipindi cha miaka mitano ijayo kikichaguliwa na kuunda serikali, kimedhamiria kuimarisha sekta za kilimo,uvuvi na ufugaji mkoani humo.
Balozi Dkt. Nchimbi katika nyakati tofauti kwenye mikutano yake ya kampeni katika maeneo hayo mbali na kusoma yaliyomo kwenye ilani ya chama hicho, yaliyolenga kuboresha na kujenga miradi ya maendeleo amesema watakwenda kujenga skimu mpya za umwagiliaji,kujenga majosho ya kuoshea mifugo, kujenga mabwawa darasa ya ufugaji wa samaki , lakini pia kutumia ndege nyuki “drones” za kisasa ili kuzuia wanyama wakali na waharibifu wakiwemo tembo ambao wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuharibu mazao.
•Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania