Muungano mkuu wa upinzani nchini Guinea-Bissau na chama cha kihistoria cha PAIGC kilichoko ndani ya muungano huo havitashiriki kwenye uchaguzi wa  uchaguzi wa rais na bunge wa mwezi Novemba mwaka huu.

Taarifa hii imetolewa kwa mujibu wa orodha ya mwisho ya vyama na wagombea iliyotangazwa jana na Mahakama ya Juu ya Guinea Bissau. 

Mahakama ya juu ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika ilitangaza kuwa kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo yaani Waziri Mkuu wa zamani Pinister Domingos Simoes Pereira hastahili kugombea katika uchaguzi huo kutokana na kuchelewa kuwasilisha taarifa zake za ugombea chini ya chama chake cha PAIGC kilichopelekea Guinea Bissau kupata uhuru kutoka kwa mkoloni Mreno. 

Mahakama ya Juu ya Guinea Bissau awali alijaribu kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi akiuwakilisha muungano wa upinzani ambao ulikuwa haujasajiliwa kwa mujibu wa sheria. 

Pereira anaongoza muungano mkuu wa upinzani nchini Guinea Bissau kwa jina la “Pai Terra Ranka”, unaojumuisha takriban vyama 10 vya kisiasa kikiwemo chama chake cha (PAIGC).

Mwishoni mwa Septemba mwaka huu Mahakama ya Juu ya nchi hiyo ilieleza kuwa  muungano wa upinzani wa “Pai Terra Ranka” haustahili kushiriki katika uchaguzi wa wabunge wa uliopangwa kufanyika Novemba 23 siku moja na uchaguzi wa rais kutokana na muungano huo kuchelewa kuwasilisha maombi. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *