Maelfu ya wakaazi wamekimbia makaazi yao kando ya bahari ya Pasifiki nchini Ufilipino wakati dhoruba ya kitropiki Fengshen ikitua na kusababisha tahadhari ya mafuriko katika pwani.

Dhoruba hiyo imeipiga manispaa ya Gubat kwenye ncha ya kisiwa cha kusini-mashariki cha Luzon na upepo mkali wa hadi kilomita 80 kwa saa, kulingana na mamlaka ya hali ya hewa. Mamlaka zilisema hakuna ripoti za haraka za uharibifu mkubwa au majeruhi, na uokoaji tayari umefanywa katika maeneo yenye hatari na jamii zilizo kwenye kitisho.

Maafisa wa maafa wamesema wakaazi wapatao 27,000 wa jimbo la Albay na kisiwa cha karibu cha Catanduanes walihamia katika maeneo salama zaidi.

Ufilipino hukumbwa na karibu dhoruba 20 na vimbunga kila mwaka, ambavyo mara kwa mara hupiga maeneo ambayo mamilioni ya watu wanaishi katika umaskini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *