Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kujenga soko la kimataifa la mazao ya kilimo katika Kata ya Mpanda Hoteli mkoani Katavi.
Soko hilo, pamoja na mambo mengine, linatarajiwa kuchochea na kukuza kipato cha wakulima wa mazao mbalimbali. Pia linatarajiwa kutumika kwa uuzaji wa mazao ya kilimo kwa mataifa jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Zambia, hasa kutokana na uwepo wa Bandari ya Karema na maboresho ya reli ya Kaliua-Mpanda yenye urefu wa kilomita 210.
Aidha, Dkt. Samia ameahidi machinjio ya kisasa na kongani za viwanda vidogo na vya kati katika wilaya zote Tanzania Bara, ili kuongeza thamani ya mazao na madini na kutengeneza ajira kwa vijana.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates