Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwalipa fidia ya wananchi wa Mpanda zaidi ya 1,200…Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwalipa fidia ya wananchi wa Mpanda zaidi ya 1,200…

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwalipa fidia ya wananchi wa Mpanda zaidi ya 1,200 waliopisha ujenzi wa miradi ya maendeleo mkoani humo.

Dkt Samia ameeleza hayo leo Jumamosi Oktoba 18,2025 wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Mpanda mkoani Katavi, katika mwendelezo kusaka kura mikoa ya Magharibi.

“Nina taarifa kuhusu uwepo wa madai ya fidia kwa wananchi waliopisha miradi ya maendeleo, wapo 243 waliopisha ujenzi wa barabara Mpanda hadi Vikonge iliyokamilika mwaka 2021.

“Pia wapo wananchi 830 wanaodai fidia kwa kupisha ujenzi wa barabara ya Mpanda hadi Sitalike ya muda mrefu mwaka 2012/13. Niwaahidi nitaiagiza Wizara ya Ujenzi kufanya upekuzi, yatakayothibitika kama ni halali yalipwe,” amesema Dkt Samia huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi.

Katika mkutano huo, Dkt Samia amesema kipindi kilichopita Serikali imeboresha uwanja wa ndege wa Katavi, ikiwemo jengo la abiria ili kurahisisha usafiri wa anga kati ya Mpanda na Dar es Salaam.

Dkt Samia amerejea ahadi yake ya kuweka kongani za viwanda vidogo na vya kati kila wilaya nchini, akiwataka viongozi wa maeneo hayo kujiandaa vyema na shughuli hiyo.

“Kama mlivyosikia Serikali ya CCM mkitupa ridhaa ya kuongoza tutatoa ajira ya watu 5,000 ya watalaamu wa afya ndani ya siku 100. Mgao huu ukitoka mkoa huu (Katavi) unakwenda kupata pia,” amesema Dkt Samia.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *