Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), DktMwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt

Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo amesema, Serikali ya Awamu ya Sita ndiyo iliyoweza kuja na mpango wa ruzuku ya mbolea kwa wakulima.

Amesema kwa Mkoa wa Ruvuma pekee kiasi cha Shilingi bilioni 100 kimetumika kwa ajili ya kulipia ruzuku na kueleza tangu kuanza kutolewa kwa ruzuku hiyo hali ya uzalishaji imekuwa ikiongezeka mwaka kwa mwaka.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wakulima na wananchi wa kijiji cha Luegu kilichopo katika wilaya ya Namtumbo mkoani ruvuma.

Mwisho amewashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kuja kujifunza juu ya matumizi sahihi ya mbolea na kueleza wanapokutana na changamoto yoyote wasisite kutoa taarifa ili kuweza kusaidia katika kutatua changamoto zinazowakabili.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *