
Wizara ya Afya ya Gaza imetangaza kuwa, miili mingi ya Wapalestina waliokabidhiwa na utawala wa Israel inaonyesha dalili za mateso makali, kunyongwa na kuporwa viungo vya mwili kama vile konea, figo na maini.
Kulingana na ripoti zilizochapishwa na Wizara ya Afya ya Gaza, kati ya jumla ya miili 120 iliyokabidhiwa, hadi hadi sasa ni miili sit tu ambayo imetambuliwa na familia zao. Baadjhi ya miili hiyo ina alama za kuraruliwa na mbwa wa jeshi la Israel na kuashiria ukali wa majeraha na ugumu wa kutambua maiti hizo.
Ripoti hiyo inasema kwamba miili mingi ilikuwa na dalili za mateso makali; baadhi ya waathiriwa walifungwa pingu walipokabidhiwa.
Wizara ya Afya ya Gaza imeeleza kwamba baadhi ya viungo, ikiwa ni pamoja na konea, figo na ini, viliondolewa kutoka kwa baadhi ya wahanga hao kitendo kilichoelezwa kama uporaji wa viungo uliofanywa utawala wa Israel.
Ripoti hizi zilichapishwa kufuatia kukabidhiwa miili na Shirika la Msalaba Mwekundu na uchunguzi wa kimatibabu huko Gaza, na zimeibua wasiwasi mkubwa wa haki za binadamu kimataifa.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Euro-Med Human Rights Monitor limewahi kutangaza kuwa, lina wasiwasi kwamba kuna uwezekano umefanyika wizi wa viungo vya maiti za Wapalestina, kufuatia ripoti zilizotolewa na wataalamu wa afya huko Gaza ambao walichunguza baadhi ya miili baada ya kuachiliwa na jeshi la Israel.