TURIN, ITALIA: Miamba ya soka ya Serie A, Juventus imebainisha Alhamisi iliyopita kwamba ipo kwenye uchunguzi mkali wa Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) kufuatia ripoti kwamba imekiuka kanuni za matumizi ya fedha.

Klabu hiyo yenye maskani yake Turin ilitangaza ripoti yake ya fedha ambayo itawasilishwa mbele ya washika dau wakuu katika kikao cha mwaka kitakachofanyika Novemba 7.

Juventus ilibainisha kwamba UEFA iliwaambia Septemba 18 kwamba kuna uchunguzi umeanzishwa dhidi yao baada ya kuonekana kama kuna udanganyifu ulifanywa juu ya matumizi ya pesa kati ya mwaka 2022 na  2025, huku kukiwa na wasiwasi kwamba hukumu inaweza kutoka mwakani.

Mabosi wa Juventus wameripotiwa kwamba wanadhani hilo linaweza kuwaweka pabaya kwenye upande wa uchumi na huenda ikafungiwa.

Uefa inazitaka klabu kuepuka haraka ya Euro 60 milioni kwa kipindi cha miaka mitatu.

Juventus, inashika namba tano kwenye msimamo wa Serie A ikiwa imekusanya pointi 12 baada ya kucheza mechi sita, ikiwa imeshinda tatu na kutoka sare tatu. Ikimilikiwa na familia ya Agnelli kwa karne sasa, Juventus ilitoa ripoti ya kuwa na hasara ya Euro 58 milioni katika ripoti yake ya mwaka wa fedha uliomalizika Juni 30. Klabu hiyo mara ya mwisho kutoa ripoti ya mwaka wa fedha iliyopata faida ilikuwa msimu 2016/2017.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *