Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) imelipa Shilingi bilioni 1.6 kwa wananchi 213 wa Kijiji cha Mpeta, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, wanaopisha ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa – SGR kipande cha sita Tabora–Kigoma.

TRC imesema ulipaji huo ni sehemu ya utekelezaji endelevu wa fidia kwa wananchi wanaoathiriwa na mradi huo.

Viongozi wa Serikali wamewataka wananchi kutumia fedha hizo kwa malengo ya maendeleo, huku baadhi yao wakishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutimiza ahadi na kuwezesha kuendelea na shughuli za kilimo.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *