Serikali ya meaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati mkoani Songwe ikiwemo upanuzi wa barabara kuu ya Tanzania na Zambia (TANZAM) kipande cha Igawa – Tunduma chenye urefu kwa kilometa 218 na ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa magari Iboya, miradi inayolenga kuboresha usafiri na uchumi wa ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Songwe, Mhandisi Suleiman Bishanga, amesema zaidi ya shilingi bilioni 300 zimetumika katika ujenzi wa barabara na madaraja.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi