Shirika lisilo la kiserikali la Bandung Afrika limeandaa mkutano wa saba wa mwaka wa Pan Afrika Diaspora, unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu jijini Arusha, ukilenga kujadili masuala muhimu ya kiuchumi ikiwemo uwekezaji, utalii katika makumbusho ya taifa, na fursa za maendeleo kwa vijana waliopo katika sekta mbalimbali.

Baadhi ya washiriki wamesema mkutano huo utakuwa jukwaa muhimu la kukuza ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa ya Afrika na mabara mengine, sambamba na kufungua milango ya ajira na uwekezaji kwa vijana na wadau wa maendeleo.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *