Dar es Salaam. Licha ya kutopata ushindi katika mechi zake mbili zilizopita, timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ bado imebaki katika nafasi yake ileile iliyokuwa mwezi Septemba katika viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) vya mwezi Oktoba.

Katika chati hiyo ya viwango vya ubora wa soka duniani, Tanzania imebaki katika nafasi ya 107 ambayo ilikuwepo mwezi Septemba.

Licha ya kutopata ushindi katika mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Zambia ambayo ilifungwa bao 1-0 na baada ya hapo ikafungwa mabao 2-0 na Iran katika mechi ya kimataifa ya kirafiki, Taifa Stars haijapanda wala kuporomoka kwenye chati hiyo.

Mambo yanaonekana kuiendea vizuri Kenya ambayo yenyewe imepanda kwa nafasi mbili katika viwango hivyo vya ubora wa soka vilivyotolewa jana.

Kenya ambayo ilikuwa katika nafasi ya 111 katika viwango vya mwezi Septemba, imepanda hadi nafasi ya 109.

Kuna anguko la nafasi moja ambalo Uganda imekutana nalo katika viwango vya ubora wa mwezi huu ambapo kutoka nafasi ya 82 iliyokuwa hapo awali, imeshuka hadi katika nafasi ya 83.

Niger ambayo mwezi uliopita iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Taifa Stars kwenye mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia, imepanda kwa nafasi tisa kutoka ile ya 117 hadi nafasi ya 108.

Niger inaonekana kubebwa na ushindi wa bao 1-0 ambao imeupata dhidi ya Zambia hivi karibuni katika mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia ambao umeifanya sasa iwe nyuma ya Taifa Stars kwa nafasi moja.

Kidunia hakujawa na mabadiliko katika nafasi ya kwanza ambayo inaendelea kushikiliwa na Hispania ingawa mabadiliko yapo katika nafasi ya pili.

Argentina iliyokuwa katika nafasi ya tatu, imepanda kwa nafasi moja hadi ya pili na Ujerumani iliyokuwa katika chati ya mwezi iliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *