“Timu zote mbili zina nafasi ya kushinda mchezo na tunashiriki hatua sawa, lakini ninachokiamini uwanjani kila kitu kipo katika ...

“Timu zote mbili zina nafasi ya kushinda mchezo na tunashiriki hatua sawa, lakini ninachokiamini uwanjani kila kitu kipo katika majukumu yake na kwa wachezaji pia, lakini timu bora itajionesha kupitia uwezo wa kiufundi, mbinu za kucheza, uwezo wa kimwili pamoja na nguvu ya ushindani”

Kocha wa Singida Black Stars Miguel Gamondi akieleza maandalizi yao kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Jumapili Oktoba 18, 2025 dhidi ya Flambeau Du Centre kwenye dimba la Prince Louis Rwagasore jijini Bunjumbura nchini Burundi

Gamondi ameongeza kuwa wako tayari kwa mchezo wa kesho na wanategemea kuwa na mchezo mzuri lakini pia wanawaheshimu wapinzani wao kwani na wao wako vizuri, ila malengo ya Singida ni kufuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo.

Na kwa upande wake Hussein Masalanga ambaye amezungumza kwa niaba ya wachezaji, amesema wamejipanga vizuri kuwakabili wapinzani wao na watazingatia kile walichofundishwa na wanaamini watakuwa na mchezo bora.

Mechi hii itachezwa kuanzia saa 10:15 jioni, na kuruka mbashara kupitia AzamSports4HD.

Imeandikwa na @davidkyamani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *