Ujenzi wa Bandari ya Karema mkoani Katavi ulioenda sambamba na ujenzi wa meli nne za mizigo utarahisisha usafiri na usafirishaji kati ya Tanzania na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Zambia.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye viwanja vya Azimio – Mpanda, Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa bandari hiyo tayari imekamilika kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 47.9. Aidha, maboresho ya reli ya Kaliua-Mpanda yenye kilomita 210 tayari yametekelezwa, kupunguza muda wa usafirishaji kutoka saa 7–8 hadi saa 2–3 pekee.

Pia, Dkt. Samia ameahidi ujenzi wa barabara ya lami kutoka Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi hadi Uvinza mkoani Kigoma kwa urefu wa kilomita 250.4, huku akiahidi kusimamia kasi ya ukamilishaji wa barabara hiyo, ambayo hadi sasa imekamilika kwa asilimia 15 kwa vipande vinne.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *