
Vyama vya upinzani vya Ivory Coast na mashirika yasiyo ya kiserikali yameshutumu marufuku ya mikutano ya kisiasa wiki moja tu kabla ya uchaguzi wa rais uliokumbwa na utata ambapo viongozi wawili vigogo wa upinzani wametolewa.
Marufuku ya miezi miwili, iliyotangazwa Ijumaa jioni na wizara ya mambo ya ndani na ulinzi, inavihusu vyama na makundi yote ya kisiasa isipokuwa wagombea watano walioidhinishwa rasmi kugombea uchaguzi wa Oktoba 25.
Haya yanajiri huku kukiwa na mvutano unaoongezeka kufuatia kuenguliwa kwa viongozi wa upinzani Laurent Gbagbo, rais wa zamani wa Ivory Coast na Tidjane Thiam. Rais wa sasa Alassane Ouattara, aliye madarakani tangu 2011, anawania muhula wa nne madarakani.
Mamia ya watu waliandamana mwishoni mwa juma lililopita mjini Abidjan huku vikosi vya usalama vikitawanya umati.