Wizara ya Afya imesema inaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha Taifa linaweka mifumo endelevu ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, hususan katika sekta ya afya.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria Wizara ya Afya, Rahibu Mashombo, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Seif Shekalaghe, wakati wa warsha iliyoandaliwa na mradi wa Choice Tanzania kwa lengo la kujadili suluhisho la mabadiliko ya tabia nchi, usawa wa kijinsia na afya ya akili kwa afya bora ya Watanzania, chini ya taasisi ya Huduma za Afya ya Aga Khan Tanzania (AKHST).
Mashombo amesema kupitia mradi wa Choice Project, Serikali imejipanga kuimarisha mikakati ya kukabiliana na athari zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambazo zimekuwa zikiathiri afya za wananchi.
Wasikilize hapa.
Mhariri @moseskwindi