Vahid Yazdanian Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Anga cha Iran ametangaza kuwa Iran imefanikiwa kurusha satelaiti sita angani kila mwaka, sambamba na kupiga hatua kubwa katika teknolojia ya kurusha satelaiti.

Yazdanian ameeleza kuwa amesisitiza kuhusu mchakato wa haraka katika uundaji na urushaji wa satelaiti zote zinazotengenezwa hapa nchini na kuashiria juu ya mustakbali mwema katika sekta hiyo. 

Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Anga cha Iran  amebainisha kuwa, juhudi za hapo awali katika miaka ya 1990 za kurusha satelaiti zinazozalishwa nchini hazikuzaa matunda, lakini azma ya wanasayansi wa Iran katika kipindi kuanzia mwaka 2000 imepelekea kurushwa kwa mafanikio ya satelaiti ya kwanza.

Amesema, satelaiti hizi zina jukumu muhimu katika kuongeza uwezo wa mawasiliano, na kuathiri moja kwa moja ubora wa maisha ya wananchi. 

Vahid Yazdanian pia amesisitiza kuwa tasnia ya anga inachangia katika usalama wa taifa na mifumo ikolojia ya kiuchumi na kwamba mkakati wa kuzidisha kasi ya maendeleo katika sekta hii unalenga kuboresha maisha ya wananchi na unaendelea kuwa kipaumbele.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *