
Maelfu ya waKenya wamejitokeza katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga mjini Bondo ambapo ibada ya mwisho ya kumuaga aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga inaendelea.
Viongozi kutoka mataifa tofauti pia wanatarajiwa kuhudhuria hafla hii itakayoongzwa na jeshi la Kenya. Odinga alikuwa kiongozi wa upinzani wa muda mrefu baada ya kuwania urais zaidi ya mara 5 bila mafanikio.
Baadaye leo jioni Odinga atazikwa katika eneo la makaburi ya familia yao, katika shamba la baba yake Kang’o ka Jaramogi, mjini Bondo, magharibi mwa Kenya.
