
China imesema uharibifu wowote unaohusiana na taasisi kama, fedha, nishati, usafiri na ulinzi kufuatia utafiti uliofanywa, ungeweza kuvuruga mawasiliano ya mtandao, mifumo ya fedha nausambazaji wa nishati.
Katika chapisho kwenye mtandao wa WeChat, wizara ya usalama wa nchi, imedai kwamba idara hiyo ya Marekani ilitumia udhaifu katika huduma za kutuma ujumbe kupitia kampuni moja ya mawasiliano ya simu kuiba taarifa nyeti kutoka vifaa vya wafanyikazi wa kituo hicho cha China mnamo 2022.
Hata hivyo haikufafanua ni kampuni gani.
Wizara hiyo pia imesema idara hiyo ya Marekani, ilitumia aina 42 za vifaa maalumu vya mashambulizi ya mtandao kulenga mifumo mbali mbali ya taasisi hiyo ya China kupenyeza mfumo muhimu wa kudhibiti nyakati rasmi kati ya 2023 na 2024.