#HABAI: Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC), imewalipa Shilingi bilioni 1.6 wananchi 213 wa Kijiji cha Mpeta Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma, wanaopisha utekelezaji wa mradi wa SGR kipande cha sita Tabora hadi Kigoma.

Hassan Mbaga ambaye ni mthamini na msimamizi wa zoezi la ulipaji fidia kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC ), amesema mradi wa SGR ni wa usanifu na ujenzi hivyo maeneo yanayohitajika kwa shughuli za mradi yamekuwa yakichukuliwa kwa hatua, hivyo kufanya zoezi la ulipaji fidia kuwa endelevu na kwaba katika awamu ya pili ya ulipaji fidia katika kipande cha sita Tabora hadi Kigoma Serikali imelipa Shilingi bilioni 1.6 kwa wananchi 213 wa Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza Mkoani Kigoma.

Akizungumzia zoezi hilo, Katibu Tarafa wa kata ya Nguruka, Wilaya ya Uvinza, Bwana Lyola Proches, ambaye katika zoezi la ulipaji fidia alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Dinah Mathaman, ametoa wito kwa wananchi waliopokea fidia husika kuzitumia fedha walizopokea kwa umakini.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *