#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limewahakikishia wananchi wa mkoa huo Amani na Utulivu siku ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, na kuwataka wajitokeze kwa wingi kutumia haki yao ya kikatiba kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP. Janeth Magomi, ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Madereva wa Bajaji, Bodaboda pamoja na magari madogo (HIACE), katika Soko Kuu la mjini Shinyanga.
Aidha amesema Jeshi hilo lipo vizuri kulinda Amani siku ya Uchaguzi Mkuu, na kwamba wananchi wasiwe na wasiwasi, bali wajitokeze kwa wingi kupiga kura na kutumia haki yao ya msingi kuwachagua viongozi wanaowataka wawaongoze kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.