#HABARI: Mbunge wa Viti Maalum mstaafu, Felista Njau, ameibuka mkoani Tabora na kuendesha kampeni kwa kutumia Baiskeli, akihamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29 na kumpigia kura Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Njau, ambaye kwa sasa amejiunga na timu ya Kampeni ya Dkt. Samia, amesema amesafiri kutoka mbali kwa lengo maalum la kuhamasisha kura za heshima kwa Dkt Samia akieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, imeweka misingi imara ya maendeleo, hususani kwa vijana.

Mbunge huyo Mstaafu amesema hatua ya kutumia Baiskeli ni ishara ya kuonyesha mshikamano na watu wa kawaida, hususani waendesha Baiskeli na waendesha Bodaboda ambao ni sehemu kubwa ya nguvu kazi ya vijana.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *