#HABARI: Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Tanga, vimeanza kuimarisha ulinzi katika maeneo tofauti, ikiwemo Mpakani Mwa nchi jirani ya Kenya, kufuatia Jeshi la Polisi kubaini kuwepo kwa mtandao wa watuhumiwa wanaodaiwa kujiandaa kufanya mandamano makubwa siku ya Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 mwezi huu, ili kuhatarisha hali ya amani na utulivu.
Hayo yamefahamika wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, akizungumza na Viongozi wa Dini, Vyama vya Siasa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo.
Kuhusu Jeshi la Polisi kubaini kuwepo kwa mtandao wa kuhatarisha hali ya amani na utulivu siku ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo Almachius Mchunguzi anafafanua kwa kina.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.