Taarifa kutoka kwa tawi hilo la kijeshi linalojulikana kama Ezzedine al-Qassam Brigades, limesema linathibitisha kujitolea kwao kikamilifu kutekeleza masharti yote yaliokubaliwa hasa usitishaji mapigano katika maeneo yote ya Ukanda wa Gaza

Pia limesema halina ufahamu wa matukio yoyote au mapigano yanayotokea katika eneo la Rafah kwa kuwa ni sehemu ya maeneo ya hatari yalio chini ya udhibiti wa vikosi vya Israel.

Kitengo cha kijeshi cha Hamas hakijakuwa na mawasiliano na wapiganaji wake Rafah 

Taarifa hiyo imeongeza kusema tawi hilo la kijeshi la Hamas halijakuwa na mawasiliano na vitengo vya Hamas vilivyosalia katika eneo hilo tangu mwisho wa kipindi cha kusitishwa kwa mapigano mnamo mwezi Machi na pia kwamba hakifahamu ikiwa wapiganaji wa vitengo hivyo bado wako hai.

Afisa mmoja wa jeshi la Israel alikuwa ameilaumu Hamas kwa mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Israel nyuma ya mstari wa vita uliokubaliwa katika makubaliano ya amani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *