Kulingana na mkuu wa IAEA Rafael Grossi, taarifa zilizoko katika shirika hilo la IAEA, zinaonyesha kuwa urani hiyo kwa kiasi kikubwa imehifadhiwa katika vinu vya nyuklia vinavyojulikana huko Isfahan na Fordo, na kwa kiasi fulani huko Natanz lakini alikiri kuwa huenda kiasi kidogo pia kilipelekwa mahali pengine.

Grossi amebainisha kuwa mnamo mwezi Juni, maeneo ya nyuklia huko Isfahan, Fordo na Natanz yaliharibiwa vibaya katika mashambulizi ya Israel na Marekani.

Grossi amesema wakaguzi wa IAEA wataweza kufikia maeneo hayo wakatu tu ambapo Iran italichukulia suala hilo kuwa la kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *