Dar es Salaam. Msanii Elizabeth Michael maarufu Lulu. Ni mtu mwenye haiba ya kipekee, mchapakazi, jasiri na mwenye kujitambua sana. Katika hili siwezi kupata mpinzani wa mawazo na kunibishia.

Ni miongoni mwa wanawake wachache walioweza kujijenga upya. Baada ya miaka kadhaa kupitia changamoto nzito sana maishani. Ni jambo linaloonesha uthabiti wake wa kiakili na kimaamuzi. 

Kwa upande wa sanaa, Lulu ni msanii mwenye kipaji asilia, hasa katika uigizaji wa hisia halisi na uhalisia wa maisha ya kila siku. Na pia kwenye mauzo mashallah bibie anauza balaa kazi zake, uliza wadosi.

Ana uwezo wa kubadilika katika majukumu mbalimbali. Acheze kama mchekeshaji, mtu mwenye huzuni, mhusika kimapenzi. Yote hufanya kwa ubora wa hali ya juu sana kuliko wasanii wengi sana.

Nje ya kamera, Lulu ni mwenye nidhamu na mwenye kujiamini. Na sasa ni mfano wa mabadiliko chanya kwa vijana wengi, hasa wanawake. Lulu wa miaka kumi nyuma siyo huyu, kilichobaki vile vile ni urembo wake.

Katuonesha kwamba binadamu anaweza kufanya makosa mengi, akaanguka, lakini akasimama na kuyajenga maisha yake upya kwa heshima na bidii. Huyu ni mfano hai na somo jepesi lenye madenti wengi wa kulisoma.

Kwa ujumla, Elizabeth Michael ni mtu mwenye nguvu ya ndani yake. Mvuto wa asili ndani yake, akili ya biashara ndani yake, na moyo wa kupambana ndani yake. Mfano halisi wa msanii ambaye amekomaa kimaisha na kisanaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *