Mgombea ubunge wa Jimbo la Nzega Mjini na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amewataka wafanyabiashara wa ndani kuchangamkia fursa ya kuuza mahindi nchini Malawi, ambayo kwa sasa inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni za mgombea wa urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Sumbawanga, Bashe amesema serikali ya Malawi imeomba kununua tani zaidi ya 200,000 za mahindi kutoka Tanzania, hivyo ni wakati muafaka kwa wafanyabiashara wa ndani kunufaika na soko hilo.

Amebainisha kuwa wizara itatoa ruhusa ya kuuza nje mahindi kwa wafanyabiashara watakaokuwa tayari kushiriki kibiashara, akionya kuwa endapo hawatajitokeza, Hifadhi ya Taifa ya Akiba ya Chakula (NFRA) litalazimika kuuza nafaka hizo.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *