Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt Samia Suluhu Hassan ameahidi kuchochea shughuli za kiuchumi na Biashara kati ya Tanzania na nchi za Congo,Burudi na Zambia kupitia bandari ya Karema ambayo Ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 47.
Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa Ahadi akiwa Uwanja wa Azimio Mpanda Katavi wakati akiomba kura na ridhaa ya wakazi wa Mkoa huo ambapo amesema anataka kuomba Biashara kubwa kati ya Tanzania na DRC ikifanyika Kwa wingi kupitia Bandari ya Karema.
Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Ujenzinwa Bandari hiyo unaenda sambamba na Ujenzi wa meli nne za mizigo katika ziwa Tanganyika.
#StarTvUpdate