Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Wakulima (AAFP), Kunje Ngombale Mwiru, amesema endapo atapewa ridhaa ya kuongoza serikali, atahakikisha anajenga kiwanda cha saruji mkoani Mwanza ili kupunguza gharama za ujenzi.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wilayani Misungwi, Kunje alibainisha kwamba atajenga mtambo mkubwa wa kuchonga kokoto ili rasilimali za mawe za mkoa zitumike katika kuboresha miundombinu, zikiwemo barabara.
Pia, alisema atalipa fidia kwa waliyojenga nyumba zao juu na chini ya miamba katika jiji la Mwanza na kusawazisha milima hiyo, kuhakikisha wananchi wanaishi kwenye maeneo salama.
✍ Innocent Aloyce
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates