Mgombea wa urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendelea kununua mahindi kutoka kwa wakulima wa Mkoa wa Rukwa na maeneo mengine nchini.
Akizungumza leo, Jumapili Oktoba 19, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Viwanja vya Kizitwe, Sumbawanga Mjini, Dkt. Samia amemuelekeza Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, kuangalia uwezekano wa kuongeza fedha kwa ajili ya kuendeleza ununuzi huo kupitia Wakala wa Chakula wa Taifa (NFRA).
Aidha, Dkt. Samia amesema serikali inaendelea kuimarisha soko la mazao nje ya nchi ili kuongeza mapato na nafasi ya kuhifadhi mahindi yanayonunuliwa kutoka kwa wakulima wa ndani.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates