María Corina Machado, kiongozi wa upinzani wa Venezuela na Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel ametoa shukrani zake za dhati kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kwa maamuzi yake ‘magumu’ wakati wa vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza.

Uungaji mkono wa kiongozi huyo wa upinzani wa Venezuela kwa utawala wa Israel unakuja wakati ambapo Umoja wa Mataifa umetoa taarifa rasmi kuthibitisha kujiri mauaji ya kimbari huko Gaza, na kukiri ukiukaji wa Israel wa sheria za kimataifa.

Netanyahu, ambaye hapo awali alisema kuwa Rais wa Marekani Donald Trump alistahili Tuzo ya Amani ya Nobel, alimpongeza Machado kwa kupokea tuzo hiyo, na kusifu juhudi zake za eti kukuza demokrasia na kuleta amani duniani.

María Machado aliwahi kumwandikia barua Waziri Mkuu wa Israel na kumtaka afanye mashambulizi ya kijeshi dhidi ya nchi yake na kutekeleza operesheni ya kuipudua serikali iliyoko madarakani.

Machado alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel 2025 kwa kile kilichodaiwa ni ujasiri wa kupigania demokrasia na uchaguzi huru licha ya vitisho. 

Machado, mkosoaji mashuhuri wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, kwa muda mrefu amekuwa akiungwa mkono na nchi za Magharibi kwa  “msimamo wa kuunga mkono demokrasia”. Hata hivyo, Venezuela na washirika wake wanamwona kama mtu mwenye kuibua migawanyiko na ambaye ametaka uingiliaji kati wa maajinabi na kuchochea machafuko.  

Kinyume na matakwa ya Alfred Nobel, mkemia wa Sweden aliyeanzisha Tuzo ya Nobel , leo hii tuzo hiyo ya kifahari imechukua sura ya kisiasa zaidi na inatumiwa kama wenzo wa kutangaza na kueneza siasa za nchi za Magharibi duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *