Mwanasiasa mkongwe na mashuhuri barani Afrika Raila Odinga atazikwa leo nyumbani kwake Bondo.

Kamati ya Kitaifa ya Kuandaa Mazishi imetangaza kuwa, ibada ya mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga itafanyika kuanzia saa tatu leo asubuhi Jumapili katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia ya Jaramogi Oginga Odinga (JOOUST), Bondo, Siaya.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Oktoba 18, 2025 jioni, mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo Naibu Rais Kithure Kindiki alisema kuwa ibada hiyo itaendelea hadi saa saba mchana.

Umati mkubwa wa watu ulikusanyika magharibi mwa Kenya jana Jumamosi kushuhudia mwili wa mwanasiasa mpendwa, Raila Odinga, katika shughuli ya maombolezo.

Kabla ya kufikishwa Bondo, mwili wa Odinga uliagwa na umati mkubwa wa waombolezaji uliojitokeza katika mji wa magharibi mwa Kenya, Kisumu. Watu kadhaa walijeruhiwa wakati wa maombolezo ya Kisumu.

Vilio vya “Baba” na “Sisi ni mayatima” vimesikika miongoni mwa maelfu ya watu waliomiminika mitaani mjini Kisumu, ngome kuu ya uungwaji mkono wa Odinga, wakati jeneza lake lilipowasili kwa helikopta katika uwanja wa jiji hilo.

Raila Odinga, mwenye umri wa miaka 80, alifariki dunia Jumatano nchini India kutokana na kile kinachoshukiwa kuwa mshtuko wa moyo, na kusababisha majonzi makubwa kote nchini, hasa katika eneo la magharibi mwa Kenya ambako kabila lake la Wajaluo linatawala.

Siku ya Alkhamisi, vikosi vya usalama vilifyatua risasi kutawanya umati uliokuwa ukisonga mbele katika uwanja wa Nairobi ambako Odinga alikuwa amewekwa kwa heshima za mwisho, na kupelekea kwa akali watu watatu kuaga dunia.

Kifo chake kimeacha pengo la uongozi katika upinzani nchini Kenya, huku wakosoaji wakimlaumu kwa kushindwa kuandaa mrithi. “

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *