Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii, Trump alimtaja Petro kama “mfanyabiashara haramu wa dawa za kulevya anayechukuliwa kuwa wa hadhi ya chini na asiyependwa na watu wengi”.

Amemuonya Petro kuchukuwa hatua dhidi ya shughuli hizo za dawa za kulevya ama Marekani itaingilia kati kwa hatua ambazo hazitakuwa nzuri.

Marekani yaishtumu Colombia kwa kutoshirikiana nayo kukabiliana na dawa za kulevya

Ujumbe huo uliochapishwa wakati ambapo Trump alikuwa katika mapumziko kwenye eneo lake la Mar-a-Lago huko

Florida, ni ishara ya hivi punde zaidi ya msuguano kati ya Marekani na mmoja wa washirika wake wa karibu katika Amerika ya Kusini.

Mnamo mwezi Septemba, serikali ya Marekani iliishutumu Colombia kwa kukosa kushirikiana nayo katika vita dhidi ya madawa ya kulevya, ingawa wakati huo ilitoa nafuu ya vikwazo ambavyo vingesababisha kupunguzwa kwa misaada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *