
Baada ya kuhesabu zaidi ya asilimia 97 ya kura, mgombea urais wa Bolivia wa mrengo wa kati-kulia ameshinda duru ya pili ya uchaguzi uliyofanyika siku ya Jumapili, Oktoba 19. Rodrigo Paz amepata 54.5% ya kura, kulingana na matokeo rasmi ya muda yaliyotangazwa na Mahakama ya Juu ya Uchaguzi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika nchi ambayo imekumbwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi baada ya miaka ishirini ya serikali za kisoshalisti, Seneta wa mrengo wa kati Rodrigo Paz, ambaye hakuna aliyetabiri kuwa angeshinda, hata hivyo ameshinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili hii, Oktoba 19 nchini Bolivia. Rodrigo Paz ambaye amemshinda mpinzani wake wa mrengo wa kulia Jorge “Tuto” Quiroga, amepata 54.5% ya kura dhidi ya 45.4% ya mpinzani wake baada ya kuhesabu zaidi ya 97% ya kura, Mahakama Kuu ya Uchaguzi (TSE) imetangaza.
Bolivia “itarejesha nafasi yake hatua kwa hatua kwenye ulingo la kimataifa […]. Ni lazima tufungue [nchi] kwa ulimwengu na kuirejesha kwenye jukumu lake,” Rodrigo Paz aetangaza baada ya kutangazwa kwa ushindi wake.
Mrithi wa familia ya kisiasa yenye ushawishi, mwanauchumi huyu mwenye umri wa miaka 58 ni mwanasiasa mwenye msimamo wa wastani na mwenye sauti ya watu wengi anayejionyesha kama mtu wa makubaliano. Anaingia madarakani katika nchi ambayo, chini ya Evo Morales, imechukua mkondo mkali sana wa kushoto: kutaifisha rasilimali za nishati, kuvunja uhusiano na Washington, ushirikiano na Venezuela ya Hugo Chavez, Cuba, China, Urusi na Iran.
Mnamo Novemba 8, Rodrigo Paz atamrithi Luis Arce ambaye hana umaarufu, ambaye ameamua kutogombea tena na ataondoka madarakani baada ya muhula wa miaka mitano uliokumbwa na mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi nchini humo katika kipindi cha miaka 40. Kushuka kwa mauzo ya gesi nje ya nchi, kutokana na ukosefu wa uwekezaji, kumepunguza akiba ya dola na kufanya sera ya gharama kubwa ya ruzuku ya mafuta kutokuwa endelevu. Kukosekana kwa fedha za kigeni kuagiza bidhaa hizo kutoka nje, uhaba wa mafuta ya petroli na dizeli umezidi kuwa mbaya, na bei imepanda sana.
Wakati mfumuko wa bei wa kila mwaka sasa ukizidi 23%, mistari mirefu ya magari yanayosubiri kujazwa mafuta kwenye vituo vya mafuta imekuwa jambo la kawaida katika nchi hii, karibu mara mbili ya Ufaransa lakini yenye idadi ya watu milioni 11.3 pekee.
Kukosekana kwa wingi wa viti bungeni
Wakati wa kampeni, wagombea wote wawili walitetea sera zinazofanana kulingana na upunguzaji mkali wa matumizi ya umma – haswa ruzuku ya mafuta – na uwazi zaidi kwa sekta ya kibinafsi. Rodrigo Paz alitetea “ubepari kwa wote” kwa kuzingatia ugatuaji wa madaraka na kubana matumizi ya fedha kabla ya deni lolote jipya. Mpinzani wake mkali zaidi, hata hivyo, alitetea uwazi kamili kwa masoko ya kimataifa na matumizi ya mikopo mipya.