EL CLASICO
Jumapili hii katika dimba la Santiago Bernabeu itapigwa EL Clasico, Real Madrid wakiwa wanaongoza msimamo wa Laliga wakiwa na alama 24 wanawakaribisha mahasimu wao FC Barcelona ambao wapo nafasi ya pili na alama 22.
Ni El Clasico ya kwanza kwa kocha Xabi Alonso akiwa anaiongoza Real Madrid.
Je, ataibuka na ushindi ama tabu kuendelea kwa Los Blancos kwani katika El Clasico mbili za mwisho Madrid kapasuka.
Mechi hii kupigwa kuanzia saa 12:15 jioni na kuruka mbashara kupitia AzamSports4HD.
Kwa kifurushi cha shilingi 28,000 unatazama mchezo huu
#ELCLASICO #FCBarcelona #RealMadrid