
Dar es Salaam. Msanii mkongwe nchini, Feruz Mrisho ‘Ferooz’ amejitapa kurudi katika gemu la muziki kama ilivyokuwa mwanzoni mwa miaka ya 2000 alipokuwa akitamba na ngoma mbalimbali ikiwamo ya Starehe.
Akizungumza na Mwananchi amesema: “Kuna ngoma zangu nyingine ambazo ziko jikoni zikishakamilika nakuhakikishia ni lazima zinirudishe kwenye enzi zangu.
“Kuna kipindi nilipotezwa na vishawishi na kuingia kwenye mambo yasiyofaa ambayo yalitaka kuniangamiza, lakini sasa nimeshajitambua na ninachodili nacho ni kupiga kazi kwa juhudi maarifa.
“Kama nilikuwa juu kwa juhudi zangu, siwezi kushindwa kurudi tena pale hasa baada ya kukaa na kutafakari nilipokosea na kugundua makosa yangu.”
Ferooz ni msanii ambaye aliwahi kutamba kitambo na nyimbo kama Jirushe, Starehe, Bisi na nyingine nyingi za kundi la Daz Nundaz kama ‘Barua’, ‘Kamanda’ na ‘Maji ya Shingo’.