#HABARI: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, amemkabidhi mjane Bi. Alice Haule hati miliki ya kiwanja ilipo nyumba pamoja na kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuanzia maisha leo Oktoba 20 jijini Dar es Salaam.

RC Chalamila pia amempa siku tano Mohamed Mstafa kujisalimisha kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa kabla ya hatua zaidi hazijachukuliwa kuhusiana na sakata la nyumba lililomhusisha na mjane Bi. Alice Haule.

Aidha, RC Chalamila amebainisha kuwa Bw. Mstafa amekuwa na maelezo yasiyoeleweka katika maelezo yake huku akiviagiza vyombo vya Dola kuendelea kumtafuta Mohamed, kwa kutumia majina ya viongozi katika maelezo yake kwa kujinasibu kuwa amekuwa na urafiki wa karibu na viongozi.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam Shukrani Kiyando amesema baada ya kupokea maoni kutoka kwenye timu iliyoundwa kufanya uchunguzi wameamua kuwa haki ya umiliki wa nyumba irudishwe kwa Bi. Alice Haule.

Akizungumza mara baada ya kupokea hati hiyo, Bi. Alice Haule amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wanyonge na pamoja na Mkuu wa Mkoa na vyombo vya habari kwa kushirikiana katika kupata haki yake.

•Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *