#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu, amesema mkoa huo umejiandaa kwa kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 unafanyika kwa amani na utulivu.
Amesema maandalizi yote muhimu yamekamilika, ikiwemo mikakati ya kudumisha usalama, kutoa elimu kwa wananchi, na kuimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wadau wa uchaguzi.
RC Babu ameyasema hayo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo.
Pia aliongeza kusema Serikali ya Mkoa huo imeweka mikakati thabiti kuhakikisha wananchi wote wanatimiza wajibu wao wa kikatiba kwa kushiriki kupiga kura.
Aidha, mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi kupuuzia taarifa zisizo sahihi zinazosambaa mitandaoni, akiwahakikishia kuwa hali ya usalama ipo shwari.
•Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania