Esmail Baqaei Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali kitendo cha utawala wa Kizayuni wa Israel cha kumtesa mwanaharakti wa haki za binadamu aliyedhihirisha mshikamano na watu wa Palestina. Baqaei amevitaja vitendo hivyo vya Israel kuwa vya ukatili, visivyo vya kibinadamu na vya udhalilishaji.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X akisema: Mienendo ya Israel inaashiria juhudi za makusudi za kuibua woga na wasiwasi na kukandamiza pande zote zinazoukosoa utawala huo kuhusu mauaji unayoyafanya katika Ukanda wa Gaza.  

Esmail Baqaei ametolea mfano mahojiano ya karibuni aliyofanyiwa Thunberg na gazeti la Sweden ambapo mwanaharakati huyo kijana alishambuliwa katika maandamano dhidi ya Israel. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia ameukosoa utawala wa Kizayuni kwa hatua zake za nyuma ya pazia kwa lengo la kupotosha fikra za waliowengi duniani. Baqaei amesema Israel inawalipa wahamasishaji iliowachagua kiasi cha dola elfu saba kwa kila chapisho ili kuficha jinai za utawala huo. 

“Ukweli ulioandikwa kwa damu isiyo na hatia hauwezi kufichwa kwa hongo au vitisho,” amesema Esmail Baqaei. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *