Israel yaruhusu tena misaada kuingia GazaIsrael yaruhusu tena misaada kuingia Gaza

Israel imeanza tena kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia katika ukanda wa Gaza baada ya hapo awali kusitisha uingizwaji wa misaada hiyo kufuatia madai kwamba kulikuwa na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya vikosi vyake.

Maafisa wa Israel wamesema  Israel imeamuru kuendelea kuingizwa kwa misaada hiyo ya kiutu katika ukanda wa Gaza kupitia kivuko cha Kerem Shalom na kupitia vivuko vingine vya zaida lakini baada ya kufanyika kwa ukaguzi wa vikosi vya Israeli na makubaliano ya kukubaliwa kuingia.
 
Hata hivyo, tamko hilo halijaweka wazi juu ya ni vivuko ngapi mpaka sasa vimefunguliwa tena kwa ajili ya kupitisha misaada hiyo ya kibinadamu.

Israel: Hamas ilikiuka makubaliano ya usitishaji wa vita

Hapo jana Jumapili, vyanzo vya usalama vya Israel vilitangaza kusitisha ufikishwaji wa misaada katika ukanda wa Gaza kwa madai kwamba kulikuwepo na ukiukwaji wa wazi wa makubaliano ya kusitisha mapigano na kundi la wapiganaji wa Hamas.

Israel Jerusalem 2025 | Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanjahu
Israel imeamuru kuendelea kuingizwa kwa misaada ya kiutu katika Ukanda wa Gaza kupitia kivuko cha Kerem ShalomPicha: Marc Israel Selem/JINI/Xinhua/picture alliance

Ni zaidi ya wiki moja sasa tangu kuanza kutelekezwa kwa mapendekezo ya Marekani yenye lengo la kuvimaliza vita katika ukanda huo vyenye miaka miwili. Rais wa Marekani Donald Trump alipoulizwa ikiwa makubaliano ya usitishaji wa vita Gaza bado yanafanya kazi alisema kipaumbele ni kuhakikisha amani inapatikana Mashariki ya Kati.

“Tunataka kuhakikisha kuwa mpango utakuwa wa amani na Hamas. Na kama unavyojua, wamekuwa wakorofi sana, na wamekuwa wakifyatua risasi, na tunadhani labda uongozi wao hauhusiki,  unajua, huenda kuna baadhi ya waasi ndani lakini kwa vyovyote vile itakavyokuwa tutashughulika ipasavyo”.

Kwa mujibu wa jeshi la Israel, wanajeshi walioko kusini mwa Ukanda wa Gaza walishambuliwa kwa kombora siku ya Jumapili, na kusababisha vifo vya askari wao wawili, na kama hatua ya kujibu mapigo Israel ilifanya mashambulizi ya anga ambayo kwa mujibu wa hospitali za ndani ya Gaza ni kwamba yamewaua Wapalestina 44.

Katika hatua nyingine jeshi hilo limetangaza pia kuendelea kukifunga kivuko cha Rafah kilichopo katika mpaka kati ya Misri na Gaza hadi pale watakapotoa taarifa ya kuufungua.

Ingawa katika kutekelezwa kwa makubaliano ya usitishaji mapigano, ufikishwaji wa misaada umeongezeka na sasa malori 600 ya misaada yanaruhusiwa kuingia Gaza kwa siku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *