
Idara ya Huduma ya Siri ya Marekani imethibitisha kuwa imegundua jukwaa linalotiliwa shaka la kufyatulia risasi karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Palm Beach likiwa na uwezo wa kuona moja kwa moja mahali ambapo kwa kawaida Rais Donald Trump hutokea kwenye Air Force One.
Taarifa ya msemaji wa Secret Service, Anthony Guglielmi, imesema kuwa “Polisi ya Federali ya Marekani, FBI, sasa inaongoza uchunguzi kufuatia ugunduzi huo.”
Huduma ya Siri ya Marekani imeeleza kuwa “muundo wa jukwaa la kufyatulia risasi unaruhusu kuona vyema jinsi Trump anavyotoka kwenye Air Force One kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Palm Beach.”
Maafisa wamesema kwamba “maajenti waligundua eneo hilo Alhamisi iliyopita,” na kuongeza kuwa “FBI kwa sasa inaongoza uchunguzi.”
Mkurugenzi wa FBI, Kash Patel, ameeleza kuwa “hakuna mtu aliyetambuliwa hadi sasa kuwa amehusishwa na jukwaa hilo.”
Palm Beach iko katika jimbo la Florida kusini mashariki mwa Marekani. Uchunguzi huo unakuja wiki kadhaa baada ya Ryan Roth kukutwa na hatia ya kujaribu kumuua Trump katika uwanja wa gofu wa Palm Beach, ambapo alitengeneza eneo la kufyatulia risasi katika vichaka karibu na uzio wa eneo hilo.