Jukwaa la Wakurugenzi Wakuu wa Makampuni Tanzania (CEOrt) limekutana na wadau kutoka serikali, sekta ya fedha, na kilimo jijini Dodoma kujadili njia bora za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia mpango wa Masuluhisho Yanayotegemea Asili (Suluhisho Zinazotegemea Asili (NbS).

Mkutano huo, ulioandaliwa kwa ushirikiano kati ya CEOrt, Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN), na Mpango wa Ukuaji wa Kilimo katika Ukanda wa Tanzania (AGCOT), umeangazia namna mpango huo kama kama upandaji miti, urejeshaji wa udongo na uhifadhi wa maji, unavyoweza kusaidia sekta ya kilimo kuwa endelevu na yenye ushindani zaidi.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Thomas Chali, amesema serikali inaendelea kuhimiza matumizi ya njia hizi kama sehemu ya juhudi za kitaifa za kupunguza hewa ukaa.

Naye Meneja Miradi wa CEOrt, Hawa Urungu amesema jukwaa hilo linaendelea kuhamasisha sekta binafsi kuunganisha masuala ya mazingira katika mipango yao ya biashara.

Kwa ujumla, kikao hicho kimeonesha kuwa mabadiliko ya tabianchi si tishio pekee, bali ni fursa ya kuimarisha uchumi endelevu na kuleta maendeleo ya kijani nchini Tanzania.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *