Jumamosi hii, Wananchi Yanga SC watakuwa dimba la Benjamin Mkapa wakiwakaribisha Silver Striker kutoka Malawi, mechi ya marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mechi hii itapigwa kuanzia saa 11:00 jioni na kuruka mbashara kupitia AzamSports3HD.
Wananchi wataingia katika mchezo huu wakisaka ushindi wa zaidi ya goli moja ili kutinga hatua ya makundi ya michuano hii.
Jumapili, Mnyama Simba SC atawakaribisha Nsingizini kutok Eswatin mechi ya marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mechi hii itapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa kuanzia saa 10:00 jioni na kuruka mbashara kupitia AzamSports1HD.
Mnyama ataingia katika mchezo huu akiwa na mtaji wa magoli matatu.
Kwa kifurushi cha shilingi 28,000 unatazama michezo hii.
#CAFCL #Azamtvsports #YangaSC #SimbaSC