Tukio hilo lilitokea Jumapili majira ya saa tatu asubuhi kwa saa za Ufaransa, ambapo wahalifu hao waliingia katika jumba hilo lililoko katikati ya mji mkuu wa Ufaransa na kuiba vitu kadhaa vya sanaa na vito vyenye thamani kubwa kabla ya kutoroka kwa kutumia pikipiki.

Polisi wa  Ufaransa  wamesema watu hao wanasakwa vikali. Jumba hilo maarufu zaidi duniani limetangaza kufungwa kutokana na hali ya dharura.

“Musée du Louvre” ni Makumbusho maarufu duniani inayotembelewa na watu wengi kutoka kila pembe ya dunia ambapo miongoni mwa mambo mengine, umaarufu wake ni  kutokana na uwepo wa mchoro wa Monalisa uliochorwa na msanii mkubwa duniani Leornado Da Vinci.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *