
Friedrich Merz amesema chama chake kitaweka wazi tofauti za msingi kati ya CDU na AfD, akisisitiza kuwa hawatashirikiana nao kisiasa.
“Sio mambo madogo tu yanayotutenganisha. Tunatofautiana na AfD kwa masuala ya msingi na imani za kisiasa,” amesema Merz.
Chama cha AfD, ambacho kinapinga Umoja wa Ulaya na uhamiaji, kimepata umaarufu mkubwa na sasa kinaongoza kwenye kura nyingi za maoni.
Katika majimbo ya Saxony-Anhalt na Mecklenburg-Vorpommern, chama cha AfD kinatarajiwa kushinda kwa kishindo, hali inayozua mjadala ndani ya CDU kuhusu uwezekano wa ushirikiano. Lakini Merz amesisitiza: “AfD haitaki tu kubadilisha sera bali wanataka nchi tofauti kabisa.”
Majimbo mengine yanayotarajiwa kupiga kura mwaka 2026 ni Berlin, Baden-Württemberg na Rhineland-Palatinate.