Mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nuru Kashakali, amewahakikishia wananchi wa kata ya Itebula kuwa atahakikisha changamoto ya kituo cha afya na uhaba wa madawati inamalizika endapo watampa ridhaa ya kuwa mbunge wao.
Kashakali alitoa ahadi hiyo wakati akihutubia wananchi wa eneo hilo katika mwendelezo wa kampeni zake za ubunge wa jimbo la Kigoma Kusini, akisisitiza kuwa ana dhamira ya dhati kuboresha huduma za kijamii, hususan sekta ya afya na elimu.
✍ Jacob Ruvilo
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates