Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka wanaobisha kuhusu mkakati wake wa kuanzisha kongani za viwanda kila Wilaya, wakaangalie kilichofanywa na Serikali yake mkoani Mtwara.
Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumapili Oktoba 19, 2025 alipozungumza na wananchi wa Simbawanga mkoani Rukwa katika mkutano wake wa kampeni za urais.
Amesema katika miaka mitano ijayo, Serikali yake itahakikisha inaanzisha kongani za viwanda ili vitumike kuongeza thamani mazao yanayozalishwa katika eneo husika.
“Kuna watu wanaweza wakasema hizo ni stori tu haiwezekani, nataka kuwaambia tumeanza kule Mtwara kwenye korosho. Kuna eneo kubwa ambalo ni kongani ya viwanda vya kubangua korosho.
“Tulikuwa tunasafirisha korosho na Maganda yake, kumbe tunasafirisha kazi, nishati na mambo mengi, sasa watac Hakata hapa yale yote wanayoyapata kwao yapatikane hapa hapa ndani ya nchi,” amesema Dkt Samia.
#StarTvUpdate