Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi mjane Alice Haule hati ya umiliki wa nyumba waliyoimiliki na marehemu mumewe Justice Rugaibura, iliyokuwa katika mgogoro na Mohamed Mustapha. Nyumba hiyo yenye namba 819, ipo eneo la Mikocheni, wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo imekuja baada ya kamati maalum iliyoundwa kwa ushirikiano na wataalamu wa ardhi kubaini kuwa taratibu za uuzaji wa nyumba hiyo hazikufuatwa ipasavyo, hivyo kurejesha haki kwa mmiliki halali.
✍Joseph Mpangala
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates